Simba wa Tsavo

Mwka 1898, simba wawili wa Tsavo waliua watu 135 katika ujenzi wa reli ya Uganda-Kenya. Simba hawa waliuliwa na Kanali J. H. Patterson aliyekuwa anasimamia mradi huo. Advertisements

Omo Twiga Mweupe Kutoka Tanzania

Kutana na Omo, twiga mweupe kutoka Tanzania.  Wakati akiwa mdogo, Omo alikuwa gunzo kutokana na kuonekana kwake kiurahisi na kuwindwa na wanyama wakali pamoja na majangili.

Julius Yego ‘Mr. Youtube Man’

Mkenya Julius Yego aliyeshinda michezo ya Olympic ya kutusha mkuki, alijifunza mchezo huo kupitia Youtube. Ameweka rekodi ya Afrika na ya Jumuiya ya Madola katika mchezo huo. 

John Akhwari

“Nchi yangu haikunituma maili 5,000 kuanza mbio, ilinituma maili 5,000 kumaliza mbio hizi. ” – John Akhwari. Mtanzania huyu aliumia katika mbio za Olympics mwaka 1968, lakini hakukata tamaa, aliendela hadi mwisho.

Joseph Kibweteere

17 Machi 2000, waumini zaidi ya 500 walijiua katika kanisa dogo lililokuwa linaongozwa na Joseph Kibweteere. Inasemekana Kibweteere yupo hai na amejificha huko nchini Malawi. 

Fela Kuti alioa wanawake 27

Mwaka 1978, Fela alioa wanawake 27 katika harusi moja. Mwaka 1985, aliwaacha wake zake wote na kusema ‘ndoa inaleta wivu na ubinafsi’.

D’banj Alikuwa Mlinzi

Mwaka 2001, D’banj alienda Uingereza na kufanya kazi ya ulinzi. Akiwa huko alikutana na Don Jazzy na kwa pamoja waliendelea na shighuli za muziki. #IpendeAfrika #JifunzeKilaSiku

Piramidi za Sudani

Nchi ya Sudani ina pitamidi nyingi kuliko sehemu nyingine duniani. Piramidi hizi ni ndogo kwa ukubwa ukilinganisha na zile zilizopo Misri. 

Luanda, Angola

Mji wa Luanda uliopo Angola, umetajwa mara 2 kama mji wenye gharama zaidi duniani kwa wageni. Pamoja na hilo, 53% ya wakazi wa Luanda wanaishi katika umasikini. 

Trevor Noah

Trevor Noah ndio mchekeshaji aliyefanikiwa zaidi kutoka Afrika. Kwa sasa Trevor Noah anatangaza kipindi maarufu cha ‘The Daily Show’ huko Marekani.